Muasisi wa University of Bagamoyo, Dr. Sengondo Mvungi afariki dunia.
Dr. Mvungi - The former DVC - ARC |
MWASISI wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo(UB), Dk.Adrian Sengondo Mvungi amefariki
dunia leo katika Hospitali ya Milpark
nchini Afrika Kusini alikokuwa amepelekwa kwaajili ya matibabu zaidi.
Akithibitisha kutokea kwa kifo hicho cha Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba, mtoto mkubwa wa marehemu ambaye ni Mkuu wa Shule ya Sheria wa (UB),
Dk.Natujwa Mvungi alisema alifarki saa 9:30 Alasiri katika hospitali hiyo ambako aliamishiwa
Novemba 8 mwaka huu, akitkea katika wodi ya wagonjwa mahututi ya Taasisi ya
Mifupa Moi Dar es Salaam ambako alilazwa
tangu Novemba 3 mwaka huu na kwamba msiba utakuwa nyumbani kwa marehemu Kibamba.
Itakumbukwa kuwa usiku wa kuamkia Novemba 3 mwaka huu,watu wanaosadikiwa
kuwa ni majambazi walivamia nyumbani kwa Dk.Mvungi huko Kibamba Kata ya Mpiji
Magohe ambaye kabla kuteuliwa kuwa
Mjumbe wa Tume hiyo alikuwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo na kumjeruhi vibaya kwa mapanga usoni na
kichwani na kumsababishia kupoteza fahamu na kisha kukimbizwa katika Hospitali
ya Tumbi usiku huo wa saa saba na kisha kuamishiwa katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili.
Dk.Mvungi ameacha mke aitwaye Anna na watoto wa tano.Alizaliwa Novemba Mosi
mwaka 1952.Mwaka 1994 alitunukiwa Shahda yake ya Udaktari katika fani ya Sheria
katika Chuo Kikuu cha Hambury ,Ujerumani.Mwaka 1987 aliipata shahada ya sheria ya pili katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na
mwaka 1981 alipata shahada yake ya kwanza
UDSM.
DK.Mvungi hadi umauti unamkuta alikuwa ni Mjumbe wa Bodi ya Kituo ya Kutetea
Haki za Binadamu(LHRC), mwaka 1995-2008 alikuwa ndiye mtetezi na mtafiti
mkuu wa Sheria na Haki za Binadamu katika mradi
wa kituo cha kutetea haki za wafugaji .Aliwai kuwa wakili toka LHRC
katika kesi ya Kikatiba ya kutetea wananchi wa kijiji cha Nyamuma.Mwaka
2000/2003 alikuwa Mkaguzi wa kitivo cha Sheria katika Chuo Kikuu cha Makerere
Uganda na mwaka 2003 alishika wadhika na kuwa Mkuu wa Kitivo cha Sheria UDSM.
0 comments:
Post a Comment