• University of Bagamoyo (UB) is a private university in Tanzania. It is started by the Tanzania Legal Education Trust (TANLET) and The Legal and Human Rights Centre (LHRC)

  • Generally, candidate to UB will become unique, excellent and successful leader who will govern the society through the truth in their services.

  • We must improve the ratio of high level graduates before East Africa can take off in its mission of social and economic development.

  • We must improve the ratio of high level graduates before East Africa can take off in its mission of social and economic development.

  • This is slide 5 description. this is a place where the remarks from the chairman on the university in general will be put. Go to Edit HTML and find this replace with proper ...

  • This is slide 5 description. this is a place where the remarks from the chancellor on the university in general will be put. Go to Edit HTML and find this replace with proper ...

Monday 9 December 2013

1st University of Bagamoyo Graduation Ceremony

Posted by University of Bagamoyo On 21:45 No comments

MAHAFALI YA CHUO KIKUU CHA BAGAMOYO(UB).YALIVYOFANA.MAKAMU WA RAIS WA TANZANIA DK.GHARIB BILAL ALIKUWA MGENI RASMI

 
Mahafali hayo yaliyofanyika Katika UKUMBI wa Makumbusho ya Taifa Dar es Salaam,Desemba 7 Mwaka 2013 AMBAPO Makamu wa Rais Tanzania,Dk.Mohammed Gharib Bilal alikuwa mgeni rasmi. Katika picha mbalimbali anaoneka Happiness Katabazi akipewa mkono wa pongezi na Makamu wa Rais Dk.Bilal.Kwani Happiness alitangazwa Kuwa mwanafunzi aliyofanya vizuri kuliko wanafunzi wote kwa ngazi ya Stashahada a Sheria.katabazi HIvi sasa ni mwanafunzi wa shahada ya Sheria ya chuo hicho Cha UB.
 
picha za tukio bofya hapa

Tuesday 12 November 2013

R.I.P Dr. Sengondo Mvungi.

Posted by University of Bagamoyo On 21:18 No comments
Muasisi wa University of Bagamoyo, Dr. Sengondo Mvungi afariki dunia.

Dr. Mvungi - The former DVC - ARC

MWASISI wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo(UB), Dk.Adrian Sengondo Mvungi amefariki dunia leo  katika Hospitali ya Milpark nchini Afrika Kusini alikokuwa amepelekwa kwaajili ya matibabu zaidi.

Akithibitisha kutokea kwa kifo hicho cha Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, mtoto mkubwa wa marehemu ambaye ni Mkuu wa Shule ya Sheria wa (UB), Dk.Natujwa Mvungi alisema alifarki saa 9:30 Alasiri  katika hospitali hiyo ambako aliamishiwa Novemba 8 mwaka huu, akitkea katika wodi ya wagonjwa mahututi ya Taasisi ya Mifupa Moi  Dar es Salaam ambako alilazwa tangu Novemba 3 mwaka huu na kwamba msiba utakuwa nyumbani kwa marehemu Kibamba.

Itakumbukwa kuwa usiku wa kuamkia Novemba 3 mwaka huu,watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi walivamia nyumbani kwa Dk.Mvungi huko Kibamba Kata ya Mpiji Magohe  ambaye kabla kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Tume hiyo alikuwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo  na kumjeruhi vibaya kwa mapanga usoni na kichwani na kumsababishia kupoteza fahamu na kisha kukimbizwa katika Hospitali ya Tumbi usiku huo wa saa saba na kisha kuamishiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Dk.Mvungi ameacha mke aitwaye Anna na watoto wa tano.Alizaliwa Novemba Mosi mwaka 1952.Mwaka 1994 alitunukiwa Shahda yake ya Udaktari katika fani ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Hambury ,Ujerumani.Mwaka 1987 aliipata shahada ya sheria  ya pili katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mwaka 1981 alipata shahada yake ya kwanza  UDSM.

DK.Mvungi hadi umauti unamkuta alikuwa ni Mjumbe wa Bodi ya Kituo ya Kutetea Haki za Binadamu(LHRC), mwaka 1995-2008 alikuwa ndiye mtetezi na mtafiti mkuu  wa Sheria na Haki za Binadamu  katika mradi  wa kituo cha kutetea haki za wafugaji .Aliwai kuwa wakili toka LHRC katika kesi ya Kikatiba ya kutetea wananchi wa kijiji cha Nyamuma.Mwaka 2000/2003 alikuwa Mkaguzi wa kitivo cha Sheria katika Chuo Kikuu cha Makerere Uganda na mwaka 2003 alishika wadhika na kuwa Mkuu wa Kitivo cha Sheria UDSM.

Tuesday 22 October 2013






Na Happiness Katabazi
NENO ‘watetezi wa haki za binadamu’ bila shaka siyo neno geni kwa masikioni mwa watu. Neno hilo limekuwepo kwasababu linatumiwa na watu wanaojitambulisha kuwa wao ni watetezi wa haki za binadamu ndani na nje ya Tanzania.

Kwa upande fulani watetezi hao wa haki za binadamu wamekuwa wakifanyakazi nzuri ya kuwaelekeza wananchi wasiyojua haki zao jinsi ya kuzidai kwa kufuata utaratibu na mwisho wa siku wanancho hao wanaozingatia ushauri wa watetezi hao wa haki za binadamu wamekuwa wakifanikiwa.

Lakini kwa upande mwingine kuna makundi ya watu wanaojitambulisha kuwa ni watetezi wa haki za binadamu kwanza hawana hata elimu ya kujua haki za binadamu ni zipi, zinadaiwa kwa njia zipi na wengine wamekuwa wakijifanya watetezi wa haki za binadamu kumbe wanatumia ngao hiyo kujificha kumbe ni wanachama wa vyama vya siasa na wakati wakiamasisha watu kudai haki zao wamekuwa wakipenyeza ajenda zao za kiitikadi jambo ambalo siyo sahii.

Hili kuondokana na wimbi la wanaharakati ucharwa ambao kadri siku zinavyozidi kusonga mbele hapa nchini linazidi kushamili,na ambapo kama wimbi hilo halitadhibitiwa Tanzania inaweza kujikuta inaingia kwenye machafuko kwa kisingizio cha baadhi ya wanaharakati wasiyo na elimu za ki uhanarakati kila kukicha kutoa matamko katika jamii ambayo wakati mwingine matamko hayo yanapotosha jamii na kuleta mivutano baina ya wananchi na serikali,  Chuo Kikuu cha Bagamoyo Dar es Salaam (UB), kinachoongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo Profesa Costa Ricky Mahalu kwa kushirikiana na Taasisi isiyoyakiserikali ya nchini Kenya , Akiba Uhaki imezindua mafunzo ya kuwanoa wale wote wanaojiita wanaharakati na wale wanye ndoto ya kuwa wanaharakati yatakayo chukua miezi sita chuoni hapo kwaajili ya kuwafundisha watetezi hao wa haki za binadamu kwanza kuzifahamu haki hizo za binadamu ni zipi, zinadaiwaje, na kisha waende kwenye jamii kuielimisha jamii jinsi ya kuzidai haki hizo kwa njia ya amani na utulivu na siyo maandamano yasiyo na vibali wala ghasia.

Tumeshuhudia baadhi ya watu wanaojiita wanaharakati wakiwachochea wananchi kudai haki kile wanachoona ni haki yao kwa kuamua kupambana na vyombo vya dola na mwisho wa siku wananchi hao wanajikuta wakiambulia kupata madhara ya kupata vigipo au kufikishwa mahakamani kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya maandamano haramu,kuzuia polisi wasifanyekazi yao na kufanya mikusanyiko haramu.Na wananchi hao wakipata madhara hayo,wale watu watu wanaojiita ni wanaharakati ambao walikuwa wakiwatuma kufanya hivyo, wao ukaa pembeni.
  
Mbali na maelezo , mwandishi wa makala hii anasimulia hotuba zilizotolewa katika uzinduzi wa program ya Akiba Uhaki inayotolewa na Chuo Kikuu cha Bagamoyo kwaajili ya kuwaonea watetezi wa haki za binadamu siku ya uzinduzi wa program hiyo uliofanyika Jumatatu usiku katika chuo hicho kilichopo Kawe Beach Dar es Salaam , ambapo Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mercy Sila alitoa hotuba yake kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza.

Sila alisema serikali inakipongeza  Chuo Kikuu cha Bagamoyo(UB), kwa uamuzi  wake wa kuanzisha kozi ya kuwanoa watu wanaojitambulisha kuwa wao ni watetezi wa haki za binadamu katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwasababu kozi hiyo itasaidia  watetezi wa haki za binadamu kufahamu wanachokifanya katika jamii na kwamba kozi hiyo inakuwa ni ya kwanza kutolewa hapa nchini.


Sila alisema program hiyo inaendeshwa na Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB) na kufadhiliwa taasisi ya kiraia ya  Haki Uhaki yenye makao makuu yake nchini Kenya, tayari imeishapata wanafunzi kumi  toka nchi za Tanzania,Kenya,Uganda,Rwanda,Burundi  na kwamba masomo hayo yatakuwa yakitolewa kwa miezi sita na kuwataka wale wote wanaojiita wanaharakati hapa nchini wafike katika chuo hicho ili waweze kufundishwa kwanza jinsi ya kufahamu haki za binadamu ni zipi ,na haki za kijamii ni zipi na hao wanadamu wanatakiwa wazitii sheria za nchi wakati wakizidai hizo haki zao bila shuruti.

“Tumeona katika mataifa ya wenzetu vurugu kila kukicha na hata hapa nchini kuna baadhi ya watu wanaojiita ni watetezi wa haki za binadamu na wamekuwa wakitumia kinga hiyo kupotosha ukweli wa mambo ambayo yanafanywa na serikali zao kwa kisingizio kuwa wa ni watetezi wa haki za binadamu wakati hata elimu ya kutetea hizo haki za binadamu hawana …leo serikali inapenda kupongeza program hii kwani itasaidia sana kuondoa mivutano na malumbano baina ya watetezi wa haki za binadamu na serikali kwani  mtu atakayepata elimu hii atakuwa ameelimika na kufahamu haki za binadamu zinapaswa zidaiwe kwa kutumia amani”alisema Sila.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo, Profesa Costa Ricky Mahalu aliishukuru serikali kwa kukubali kuja kuzindua program hiyo kwani programu ni yakwanza kutolewa katika vyuo vya hapa nchini na program hiyo itawezesha kuondoa malumbano baina ya serikali na watetezi wa haki za binadamu kwani ni wazi hivi sasa kumeibuka watu wanaojitambulisha kuwa ni watetezi wa haki za binadamu wakati hawana hata elimu ya huo utetezi wa haki za binadamu na wamekuwa wakitoa baadhi ya matamko ambayo  hayana mantiki katika suala zima la utetezi wa haki za binadamu hali ambayo alisema ikiachwa iendelee italeta madhara katika jamii.

“UB inaamini katika elimu zaidi…hivyo UB imeona ni jambo jema kuanzisha program hiyo ya mafunzo ya muda mfupi kwa wale wote wanaotaka na wanajiita watetezi wa haki za binadamu waje kufundishwa masuala hayo na waadhiri waliobobea katika eneo hilo la masuala ya haki za binadamu”alisema Profesa Mahalu.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Bagamoyo  Dk.Natujwa Mvungi ambayo program hiyo ya Akiba uhaki inatolewa chini ya kitivo chake alisema   jumla ya wanafunzi 10 toka katika nchi tano za jumuiya ya Afrika Mashariki  wa kozi ya Akiba Uhaki ,wameishafika hapa nchini na wanaanza mafunzo hayo kwa muda wa miezi sita kuanzia wiki hii chuo hapo na kwamba wanafunzi hao wamefadhiliwa ada ya kusoma kozi hiyo na taasisi isiyo ya kiserikali yenye makao makuu yake nchini Kenya ya Akiba uhaki na kuwataka wale wote wanaojiita ni watetezi wa haki za binadamu  wakati hawana elimu ya kuonyesha wamefudhu kozi hiyo,wasisite kuja kupata elimu hiyo chuo hapo.

Aidha Mratibu wa Programu hiyo toka Taasisi ya Akiba Uhaki ya nchini Kenya, Kempta Ombati alishukuru chuo cha UB, kukubali kushirikiano nao kutoa mafunzo hayo ambayo yasaidia nchi za Afrika Mashariki kuondokana na watu wanaojiita kuwa ni wanaharakati wakati hawana elimu ya kuzijua haki wanazozitetea na wajibu na kwamba taasisi yake ndiyo imetoa ufadhili kwa wanafunzi hao kumi wanaotoka nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuja kuudhulia kozi hiyo  katika chuo Kikuu cha Bagamoyo na kwamba mafunzo hayo ni ya kwanza kutolewa katika vyuo vya hapa nchini na kwamba taasisi yao itaendelea kutoa ufadhili.

Yaliyojiri maadhimisho siku ya kuzaliwa kwa UB

Posted by University of Bagamoyo On 23:29 No comments












Tuesday 1 October 2013

Fellowship program at UB

Posted by University of Bagamoyo On 12:22 No comments
Fellowship program at UB

The Akiba Uhaki Foundation in collaboration with the University of Bagamoyo invites applications for the Human rights and Social Justice Fellowship program starting September 2013. The fellowship program will be held at The University of Bagamoyo Dar es Salaam Tanzania.
 Click here for Application forms

Postgraduate Overview

Posted by University of Bagamoyo On 12:20 No comments
Post Graduate School of Science and ICT
  • The Post graduate School of Science offers Post Graduate Diplomas, Masters and PhD in Science and ICT with governance.
  • The Post Graduate School of Law & Governance offers post graduate programmes that include Post Graduate Diploma in Law and Governance, Master of Laws and Governance and Doctor of philosophy of Laws and Governance.
The Post Graduate Leadership Training Programme
This is an elite leadership training programme aimed at training graduate students as leaders irrespective of their Alma matter. The objective of this programme is to improve leadership quality in Africa and the world generally. The post graduate products of UB shall be professional leaders capable of good leadership and innovation within competitive global social economic development imperatives.

Site search